Dodoma FM

Waathirika janga la moto Mchinga Coplex wapewa mkono wa pole

22 September 2026, 17:42

Picha ni mkuu wa mkoa wa Dodoma mh rosemery Senyamule akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri wakitoa mkono wa pole kwa waathirika wa janga la moto sokoni hapo. Picha na Mkoa wa Dodoma.

Serikali itaendelea kuwaunga mkono wafanyabiashara hao na kuweka mazingira rafiki ya kurejesha shughuli zao za biashara.

Na Yussuph Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ametoa Shilingi laki 5 kama mkono wa pole kwa wafanyabiashara walioathirika na moto katika Soko la Machinga Dodoma.

Mhe. Senyamule amesema Serikali itaendelea kuwaunga mkono wafanyabiashara hao na kuweka mazingira rafiki ya kurejesha shughuli zao za biashara wakati marekebisho ya soko yakiendelea.

Sauti ya mh. Senyamule.