Vijana watakiwa kugeuza vipaji kuwa fursa
17 November 2026, 16:17

Mtaalamu huyo anasisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa wabunifu, kujiamini na kutumia fursa zinazopatikana katika jamii ili kukuza vipaji vyao na kuchangia maendeleo yao pamoja na taifa kwa ujumla.
Na Mwanaidi Mpetu.
Vijana wametakiwa kutambua kuwa kipaji kinapaswa kuendelezwa kupitia mafunzo mbalimbali, nidhamu na ubunifu ili kiweze kuwa na manufaa ya kugeuka kuwa fursa.
Baadhi ya wananchi wanasema kuwa vijana wanapaswa kutambua thamani ya vipaji walivyonavyo na kuvitumia kama fursa ya kujiajiri na kujipatia kipato badala ya kutegemea ajira pekee.
Wamesema vijana wanaweza kutumia majukwaa mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kutangaza kazi zao na kuwafikia watu wengi zaidi.
Kwa upande wake, mtaalamu wa masuala ya sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Bw. Maro Protas anasema kuwa kipaji kinahitaji kuendelezwa kupitia mafunzo, ubunifu, nidhamu na kujifunza mbinu za kukifanya kuwa shughuli yenye manufaa kiuchumi.