Dodoma FM

Unywaji wa pombe kupita kiasi wahusishwa na ukatili wa kijinsia

20 October 2026, 17:09

Picha ni mwanaume anayatumia pombe kwa lengo la kutuliza mawazo. Picha na mwananchi.

Unywaji wa pombe kupita kiasi umetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii, huku baadhi ya watu wakishindwa kudhibiti hisia na matendo yao wanapokuwa wamelewa. Wadau wa masuala ya maadili na familia wamesema dhana ya baadhi ya watu kuwa pombe husaidia kupunguza msongo wa mawazo inaweza kuchochea matumizi yasiyo sahihi ya kilevi na kuathiri mahusiano ya kifamilia, hali inayoweza kusababisha migogoro, vipigo na aina nyingine za ukatili.

Na Daniel Njau.

Unywaji wa pombe kupita kiasi umetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazo weza kuchangia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii

Baadhi ya wananchi wamezungumza na taswira ya habari ambapo wamesema watu wengi hudhani kuwa kunywa pombe kunasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kujikuta wakiitumia kupita kawaida hali inayo changia watu hao kufanya vitendo visivyo faa ikiwemo ukatili .

Bi. Janne Ndetabura ni mshauri wa masuala ya malezi yeye anasema ulevi uliopitiliza unaweza kumfanya mtu ashindwe kudhibiti kauli na matendo yake, ikiwemo kutumia lugha chafu anapozungumza na watu wengine.

Aidha amesisitiza umuhimu wa jamii kuwa na uelewa kuhusu madhara ya unywaji wa pombe kupita kiasi na kuhimiza matumizi yenye kiasi pamoja na kujenga tabia ya kutafuta njia salama za kukabiliana na msongo wa mawazo, ili kupunguza migogoro na vitendo vya ukatili katika familia na jamii.

Simulizi na Daniel Njau.