Dodoma FM

Vijana watakiwa kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kukuza biashara

28 October 2026, 17:18

Picha ni kijana ikitumia simujanja yenye mitandao ya kijamii kama fursa katika maisha. Picha na DW Swahili.

Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii yanaendelea kuwa fursa muhimu kwa vijana na wajasiriamali kukuza biashara zao, kuongeza wigo wa wateja na kujipatia kipato. Hivyo, vijana wanahimizwa kutumia teknolojia kwa ubunifu na uzalishaji, huku wakizingatia wajibu wao wa kulinda amani, mshikamano na utulivu wa jamii.

Na Anwary Shabani.

Vijana nchini wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kukuza biashara, kujitangaza na kujipatia kipato, badala ya kuitumia kwa vitendo vinavyoweza kuchochea vurugu na kuathiri amani na utulivu wa nchi.

Wito huo umetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya teknolojia katika kujiletea maendeleo ya kiuchumi, hususan kwa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Katika kuonesha namna mitandao ya kijamii inavyoweza kuwa chachu ya mafanikio ya kibiashara, Taswira ya Habari imezungumza na Gladis Kimario, mwanamke anayefanya biashara ya utengenezaji wa taulo na kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zake na kuwafikia wateja.

Kimario anaeleza namna matumizi ya teknolojia yanavyomsaidia kuitangaza biashara yake na kuitumia mitandao kama nyenzo ya kujitanua kiuchumi.

Simulizi na Anwary Shabani.