Ujenzi holela watajwa kuziba njia za dharura Kiteto
30 October 2026, 17:11

Ukiukwaji wa taratibu na sheria za ujenzi katika baadhi ya maeneo ya wazi na barabara zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi na magari ya dharura, ikiwemo magari ya zimamoto, umeendelea kuleta hofu miongoni mwa wakazi wa mji wa Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Na Kitana Hamisi.
Ujenzi unaokiuka taratibu za mipango miji katika baadhi ya maeneo ya wazi na njia zilizotengwa kwa matumizi ya umma umetajwa kuhatarisha usalama wa wakazi wa Mji wa Kibaya wilayani Kiteto, mkoani Manyara, kutokana na kuzibwa kwa njia zinazopaswa kutumiwa na magari ya dharura, yakiwemo ya zimamoto.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema ujenzi katika maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma umekuwa ukikwamisha upatikanaji wa njia za dharura, hali inayoweza kuongeza madhara wakati wa kutokea kwa majanga yanayohitaji uokoaji wa haraka.
Taswira ya Habari imefika katika baadhi ya maeneo na kushuhudia hali hiyo, huku wananchi wakieleza changamoto wanazokabiliana nazo na kuomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kudhibiti ukiukwaji huo.
Kwa upande wake, Msaidizi wa Sheria, Abasi Famau, ameeleza hatua zinazoweza kuchukuliwa kisheria dhidi ya wanaokiuka taratibu za ujenzi, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria za mipango miji na kulinda maeneo ya wazi pamoja na njia zilizotengwa kwa matumizi ya umma.