Dodoma FM

Vijana washauriwa kutumia talanta kuwa fursa za uchumi

13 November 2026, 16:07

Picha ni vijana wakitumia fursa zilizopo kupitia mitandao ya kijamii. Picha na Mwananchi.

Vijana wameshauriwa kujitangaza kupitia vipaji na talanta zao, kufanya kazi kwa bidii na kujiwekea malengo yanayotekelezeka, huku wakijifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa ili kuongeza ubunifu, kuimarisha uwezo wao na kujenga msingi imara wa kujitegemea kiuchumi.

Na Daniel Njau.

Vijana nchini wametakiwa kujiamini, kutambua na kutumia vipaji pamoja na talanta walizonazo kama nyenzo ya kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi, badala ya kutegemea ajira rasmi pekee kama njia ya kufikia mafanikio ya maisha.

Baadhi ya wananchi wamesema ni muhimu vijana kutambua uwezo wao, kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na kutumia fursa zinazowazunguka ili kuanzisha shughuli zitakazowawezesha kujiajiri na kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake, Bw. Hamisi Kasogo, mshauri wa masuala ya biashara na uchumi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), amesema mfumo wa elimu umekuwa ukimwandaa zaidi kijana kusoma na hatimaye kutafuta ajira, hali inayochangia baadhi yao kushindwa kubadili maarifa wanayoyapata darasani kuwa fursa za kujiajiri na kujipatia kipato.

Simulizi na Daniel Njau.