Daraja la Osterbay lafungua fursa za kiuchumi na kijamii
5 November 2026, 16:39

Daraja hilo linatarajiwa kuendelea kuwa kiungo muhimu kwa wakazi wa Mitaa ya Osterbay na Mathias, huku wananchi wakihimizwa kushirikiana katika kuhakikisha linatunzwa na kutumika kwa usalama kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Na Anwary Shabani.
Wakazi wa Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma, wamesema kuanza kutumika kwa daraja la watembea kwa miguu linalo unganisha Mtaa wa Mathias, Kata ya Miyuji, kumesaidia kurahisisha shughuli zao za kila siku pamoja na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Wakizungumza wakazi hao wamesema kabla ya kukamilika kwa daraja hilo walikabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuvuka eneo hilo, hali iliyohatarisha usalama wao na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha. Wamesema uwepo wa daraja hilo sasa umekuwa mkombozi kwao kwa kurahisisha mawasiliano na shughuli za kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Kesi Joseph, amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kutunza na kulinda miundombinu hiyo ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu na kuwaepusha na changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo hapo awali.