Dodoma FM

Kukosa usingizi wakutosha watajwa kuhatarisha afya

2 September 2026, 16:46

Kusoma pamoja na kutumia simu nyakati za usiku sababu zinazo changia mtu kukosa usingizi wa kutosha. Picha na mtandao.

Wananchi wanahimizwa kutambua umuhimu wa kupata usingizi wa kutosha na kuacha kuuchukulia kama muda wa kupoteza, kwani kulala vizuri ni sehemu ya msingi ya kulinda afya na kuongeza uwezo wa kufanya shughuli za kila siku kwa ufanisi.

Na Elizabeth Mwinuka.                                                                                 

Kukosa usingizi wa kutosha ni miongoni mwa changamoto zinazoweza kuathiri afya ya mwili, huku maisha yenye shughuli nyingi, matumizi ya vifaa vya kielektroniki na majukumu ya kila siku yakitajwa kuwa baadhi ya sababu zinazowafanya watu kutopata muda wa kutosha wa kupumzika.

Baadhi ya wadau katika jamii wamesema wamekuwa wakilala kwa muda mfupi kutokana na kuchelewa kufanya shughuli mbalimbali, kusoma pamoja na kutumia simu nyakati za usiku.

Wamesema hali hiyo imekuwa ikiwafanya kuamka wakiwa wamechoka na wakati mwingine kushindwa kuwa makini katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumzia hali hiyo mtaaalamu wa saikolojia na ushauri nasaha kutokea navet counselling center  Deborah mwangomo amesema usingizi wa kutosha ni muhimu kwa mwili kwa sababu husaidia mwili na ubongo kupata muda wa kupumzika na kujirekebisha

Aidha, mtaalamu huyo amewashauri wananchi kuweka utaratibu mzuri wa kulala na kuamka, kupunguza matumizi ya simu na vifaa vingine vya kielektroniki kabla ya muda wa kulala, pamoja na kutenga muda wa kutosha kwa ajili ya mapumziko.