Dodoma FM

Athari za kiuchumi zinavyo pelekea changamoto ya afya ya akili

22 July 2026, 16:51

Kulingana na hali ya msongo wa mawazo kwa vijana wao utumia vilevi na kuvuta bangi.Picha na Mtandao.

kwa upande wake msaikolojia mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Christopher Abuto ameshauri kuwa jamii nzima ichukue hatua ya kuyaona masuala ya maisha kuwa ni mambo ya kawaida kwa kutoweka malengo makubwa zaidi ya namna wanavyoishi na wanapokutana na magumu wazungumze na wataalam pasipo kukaa kimya.

Na Jerome John.

Wakazi wa Kata ya Ng’ong’ona  Jijini Dodoma wamezitaka Asasi  mbali mbali za kiraia kujitokeza ili kuwapa elimu ya maisha  vijana wanaoishi kwenye kata hiyo kutokana na baadhi yao  kuwa na hali ya kukata tamaa ya maisha.

Wakizungumza na taswira ya habari wakazi hao wamesema kuwa kumekuwa na vitendo vya vijana mtaani hapo kuonesha hali ya kukata tamaa kwa kukosa ajira na kuwa na maisha magumu na hivyo kujizulu na wengine kujitoa uhai.

Baadhi ya wazazi wamesema kulingana na hali ya msongo wa mawazo kwa vijana wao utumia vilevi na kuvuta bangi wakisema kuwa wanapunguza mawazo na ujikuta wakichukua maamuzi magumu ya kukatisha maisha yao.

Discussion afya ya akili