Dodoma FM

CCM yakerwa kusuasua  miradi ya Maji Dodoma

19 November 2023, 11:18 am

Picha ni wajumbe wa kamati ya siasa mkoa was Dodoma wakiongozwa na katibu wa Itikadi siasa uenezi na mafunzo mkoa was Dodoma Bw. Jawadu Mohammed wakiwa katika eneo la ujenzi wa mradi wa maji kata ya chali.Picha na Bernad Magawa.

Ikumbukwe kwamba  mwezi June mwaka huu, Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi Comredi Daniel Chongolo alifanya ziara Mkoani Dodoma na kuagiza kukamilishwa haraka kwa mradi wa maji wa kata ya chali na Ibihwa lakini mpaka sasa miradi yote imesimama kutokana na kukosekana kwa fedha za kukamilisha miradi hiyo.

Na Bernad Magawa.

Kamati ya Siasa ya Chama cha mapinduzi Mkoa wa Dodoma imesikitishwa  na kukwama kwa  miradi  ya maji inayotekelezwa ndani ya  wilaya za mkoa huo na kuahidi kufuatilia kwa undani chanzo cha kutokamilika kwake  ili wote wanaohusika kukwamisha miradi hiyo waweze kuwajibishwa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Siasa Itikati Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Dodoma Bw. Jawadu Mohamed wialayani Bahi wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipofika kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kamati hiyo ndani ya mkoa mzima wa Dodoma kuona na  kukagua miradi yote iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali baada ya kukagua Miradi ya maendeleo wilayani Bahi ukiwemo mradi wa maji katika kata ya chali unaotarajia kugharimu  Bilion 2.3 mpaka kukamilika kwake Bw. Jawadu Mohamed amesema chama hakiwezi kuona wananchi wanaendelea kuteseka kwa kukosa maji wakati  kiliahidi kusogeza huduma zote muhimu kwa wananchi.

Sauti ya Bw. Jawadu Mohamed .
Picha ni wajumbe wa kamati ya siasa mkoa was Dodoma wakiongozwa na katibu wa Itikadi siasa uenezi na mafunzo mkoa was Dodoma Bw. Jawadu Mohammed wakiwa katika eneo la ujenzi wa mradi wa maji kata ya chali.Picha na Bernad Magawa.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya  Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa huo Ndg. Samwel Malechele amesema CCM haiwezi kuvumilia kuona maelekezo ya viongozi wakubwa wa chama yanapuuzwa huku akiwaomba radhi wananchi wa kijiji cha Chali kwa kuendelea kukosa huduma ya Maji.

Sauti ya Mwenyekiti wa wazazi Dodoma.

Awali, akitoa taarifa ya mradi wa maji wa kata ya chali mbele ya kamati ya Sisasa ya Mkoa wa Dodoma,  Meneja wa Ruwasa wilaya ya Bahi Mhandisi Robart Mgombelwa amesema Mradi huo ulipaswa kukamilika Mwezi Julai mwaka huu lakini haujakamilika kutokana na kukosekana kwa fedha.

Sauti ya Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Dodoma.