Dodoma FM

Afikishwa mahakamani kwa kukutwa na dawa za kulevya

3 December 2020, 3:31 pm

Na,Zakia Ndulute,

Dodoma.

Mkazi wa Mkalama ‘A’ jijini Dodoma ENOCK JOHN [24] leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma kwa shitaka la kukutwa na madawa ya kulevya.
Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma DENIS MPELEMBWA na mwendesha mashitaka ambaye ni wakili wa serikali RACHEL TULLI amedai kuwa mnamo mwezi juni mwaka huu mshitakiwa alikutwa na madawa ya kulevya aina ya Bhangi yenye uzito wa kilogramu 248.45.
Hata hivyo Mshitakiwa amekana kutotenda kosa hilo.
Naye wakili wa serikali amesema kuwa upelelezi wa shitaka hilo tayali umekamilika na amemuomba Hakimu kutaja tena tarehe ya kusoma kesi hiyo.
Kwa upande wake Hakimu MPELEMBWA amesema kuwa dhamana ya mshitakiwa iko wazi kwa mashariti ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua, nakala ya kitambulisho cha Taifa Pamoja na kulipa bondi ya shilingi milioni mbili.
Mshitakiwa ameachiwa nje kwa dhamana baada ya mdhamini wake kukidhi vigezo vya masharti ya dhamana na shauri litasomwa Mahakamani tena Disemba 28 mwaka huu.