Dodoma FM

Hombolo Makulu walia na uchakavu wa shule

20 September 2023, 4:45 pm

Picha ni muonekano wa shule ya Msingi Hombolo Makulu iliyopo Jijini Dodoma. Picha na Twitter.

Mazingira magumu au uchakavu wa miundombinu ya shule pamoja ongezeko la wanafunzi ni moja ya changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa mtaa wa Hombolo Makulu wamelalamikia uchakavu wa miundombinu ya shule yao ya msingi hali inayo wakosesha ufanisi walimu na wanafunzi wa shule hiyo

Wamesema kuwa ubora wa mazingira ya shule unaweza kuwa kivutio kikubwa kwa mwanafunzi katika kuongeza morali wa kujifunza  pamoja na ufanisi wa kufundisha kwa walimu

Sauti za wananchi.

Aidha wameongeza kuwa uchakavu wa miundombinu hiyo ya madarasa unapelekea usalama mdogo wa kutunza dhana zao za kujifunzia

Wamesema kuwa kukosekana kwa ukarabati mashuleni unaweza  kupelekea baadhi yd watoto kukua kwa kuichukia kutokana na mazingira magumu waliyonayo shuleni

Sauti za wananchi.
Picha ni muonekano wa madarasa yaliyo chakaa katika shule hiyo iliyopo Jijini Dodoma. Picha na Twitter.

Wiliamu Mkuna mwenyekiti wa mtaa huo amesema changamoto kubwa ni uchakavu wa shule mama ya msingi kutokana na kujengwa kipindi cha miaka ya ukoloni

Mkuna amesema kuwa hata hivyo tayari shule hiyo imetengewa bajeti yake ya kujengwa upya  huku akitoa shukrani kwa Serikali kwa ujenzi wa shule ya mfano katika kitongoji cha Maheto

Sauti ya Bw. William Mkuna.