Dodoma FM

EWURA yatoa msaada wa mashuka 431 katika vituo vinne jijini Dodoma

24 June 2021, 9:38 am

Na; Mindi Joseph .

Katika kuhitimisha wiki ya utumishi wa umma mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetoa msaada wa mashuka 431 kwa vituo vinne vya afya jijini Dodoma  kwa lengo la kusaidia kuboresha huduma za afya.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo  kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Ewura Mhandisi Godfrey  Chibulunje amesema wameamua kutoa msaada huo kwa jamii lengo ni likiwa ni kurudisha kwa jamii kwa zile shughuli mbalimbali wanazozifanya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Wa Jiji La Dodoma Dkt Andrew Methody amesema msaada huo unakwenda kuchochea utoaji wa huduma bora za afya  katika vituo hivyo kutokana na jiji la Dodoma kukua kwa kasi.

Katika hatua nyingine wananchi pamoja na taasisi mbalimbali jijini Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima  ili kujiepusha na janga la virusi vya corona.

Mganga mkuu wa jiji la Dodoma Dkt.Andrew Methody amesema kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu katika jiji hili ni vyema tahadhari zikachukuliwa ili kujiweka salama.