Dodoma FM

Taasisi za vijana zakutana kujadili jinsi ya kufanya kazi pamoja

17 May 2023, 3:54 pm

Vijana wakiwa katika mkutano huo uliojumuisha zaidi ya taasisi 20 zisizokuwa za kiserikali (NGO’s) ili kupata mafunzo katika utendaji wa majukumu ya taasisi zao. Picha na Mindi Joseph.

Mkutano huo umeandaliwa na umoja wa vijana hao kwa kushirikiana na shirika la Foundation for Civil Society FCS.

Na Alfred Bulahya.

Umoja wa vijana kutoka taasisi zinazofanya kazi kwenye afua za vijana, zimekutaka jijini Dodoma kujadili namna zinavyoweza kufanya kazi kwa pamoja ili kusukuma ajenda za vijana na kufikia nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, afya na elimu.

Mkutano huo umejumuisha zaidi ya taasisi 20 zisizokuwa za kiserikali (NGO’s) ili kupata mafunzo katika utendaji wa majukumu ya taasisi zao.

Akizungumza na Dodoma Tv mwenyekiti wa umoja huo bi. Elizabeth Msuya, ameeleza lengo kuu la mkutano huo.

Sauti ya Mwenyekiti wa umoja huo.
Vijana hao wakieleza jinsi mafunzo hayo yatakavyowanufaisha. Picha na Mindi Joseph.

Awali akifungua mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya jamii idara kuu ya vijana jiji la Dodoma Bw.Mfungo Manyama amesema vijana wanapaswa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia mila na dseturi za nchi.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya jamii idara kuu ya vijana jiji la Dodoma.

Mkufunzi katika mafunzo hayo bw. Badru Juma, akabainisha sababu za mafunzo hayo kutolewa wakati huu huku baadhi ya vijana wakieleza matarajio yao baada ya mafunzo.

Sauti ya Mkufunzi katika mafunzo hayo.