Dodoma FM

Msukumo mkubwa wa maji wachangia kupasuka kwa mabomba

15 April 2024, 9:34 pm

Picha ni maji yanayo tiririka baada ya kupasuka kwa mabomba Nzuguni.Picha na George John.

Duwasa imeendelea kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya upotevu wa maji ambao husababishwa na kupasuka kwa miundombinu ya Mabomba ya maji kutokana na presha kubwa ya maji.

Na Mindi Joseph.

Msukumo mkubwa wa maji umetajwa kuchangia Kupasuka kwa miundombinu ya mabomba ya maji Nzuguni  na kuchangia upotevu wa maji ambao unaathiri upatikanaji wa huduma hiyo.

Dodoma Tv imezungumza na Kaimu  Mkurugenzi wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi Benard Rugayi ambapo amesema changamoto hiyo imekuwa ikijitokeza lakini wamekuwa wakichukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hiyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira DUWASA .
Picha ni Mtaa wa Nzuguni B unaopatikana katika jiji la Dodoma.Picha na George John.

James Rioba ni Mhandisi wa Maji kutoka DUWASA anasema wanatimu ya kuhakikisha pindi wanapopokea taarifa za mabomba ya maji kupasuka wanaitatua mara moja na kuhakikisha maji yanawafikia wananchi husika.

Sauti ya James Rioba Mhandisi wa Maji kutoka DUWASA.