Dodoma FM

Wakulima wa Nyanya watamani viwanda vya kusindika zao hilo

5 July 2023, 5:48 pm

Picha ni Bidhaa ya nyanya ikiwa imepangwa sokoni kwaajili ya kuuzwa. Picha na Tadei Tesha.

kwa sasa wastani wa bei ya nyanya sokoni ni kati ya shilingi 2000, 2500 hadi 3000 kwa ujazo wa sado moja.

Na Tadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wakulima wa nyanya katika soko kuu la majengo jijini Dodoma wameiomba serikali kutengeneza viwanda kwa ajili ya kuuzia bidhaa za nyanya kutokna na bidhaa hiyo kuharibika pale zinapokosa wateja.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakulima hao ambapo wamesema kuwa kwa sasa ni msimu wa bidhaa hiyo ambapo ipo kwa wingi sokoni inawalazimu kutupa bidhaa hizo pale wanapokosa wateja hali ambayo inawapa ugumu.

Sauti za Wafanyabiashara.
Maboksi yaliyo hifadhiwa Nyanya ambazo zimetoka shambani na tayari zimeshushwa sokoni. Picha na Thadei Tesha.

Aidha pamoja na mambo mengine wameiomba serikali kuwajengea viwanda kwa ajili ya kusindika bidhaa za nyanya kwa lengo la kuepuka kutupwa kwa bidhaa hiyo kiholela pindi zinapoharbika kwa kukosa wateja.

Sauti za wafanyabiashara.