Dodoma FM

Wananchi Hombolo Makulu walia na fidia ndogo

2 March 2021, 1:07 pm

Na, Alfred Bulahya,

Dodoma.

Wananchi wa mtaa wa Mkoyo Makulu Kata ya Hombolo Bwawani wameiomba Serikali, kuwaongezea pesa za fidia zinazotolewa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa eneo la hifanyi ya Kinyami iliyopo Kijijini hapo.

Hatua hiyo inakuja wakati wananchi wakijiandaa kuondoka kwenye eneo hilo ili kupisha upanuzi wa hifanyi hiyo huku wakiiomba Serikali kuwaongezea fedha hizo kutoka 250,000 kwa ekari wanazotarajia kupewa, hadi kufikia kiwango cha 600,000 na kuendelea.

Wakizungumza na Taswira ya habari Kijijini hapo wananchi hao wamesema wameupokea vyema mradi huo wakiamini utaleta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Benjamin Eliah, amekiri kuwepo kwa zoezi hilo huku akidai kutoridhishwa na mchakato unavyokwenda kutokana kutowekwa wazi kwa baadhi ya mambo.

Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Bw.Asedi Ndajilo amesema tayari ameliwasilisha jambo hilo kwa mkuu wa Wilaya ya Dodoma Bw.Josephat Maganga na kwamba kwa sasa wanasubiri majibu kutoka mamlaka za juu.