Dodoma FM

Serikali yaombwa kutunga sheria kali dhidi ya wanaotelekeza familia

19 September 2023, 2:46 pm

Mkazi wa Bahi akizungumza katika mjadala wa wazi uliofanyika wilayani humo katika eneo la Bahi Sokoni. Picha na George John.

Hayo yamaebainishwa na wananchi wilayani Bahi wakati wakizungumza katika mdahalo wa wazi ulioandaliwa na kipindi cha Sakuka na kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Alfred Bulahya.

Wananchi wilayani Bahi mkoani Dodoma wameiomba serikali na bunge kutunga sheria kali kuhusu watu wanaotelekeza familia ili kusaidia kukomesha vitendo vya utelekezaji wa familia.

Wananchi hao wamesema licha ya uwepo wa sheria kadhaa ikiwemo dawati la jinsia na watoto bado sheria hizo zimekuwa hazisimamiwi ipasavyo na kusababisha sintofahamu baina yao kuhusu nani anapaswa kupeleka malalamiko yake katika dawati hilo.

Sauti za wananchi.
Wakazi wa Bahi Sokoni wakiwa katika mjadala wa wazi ulio fanyika wilayani humo katika eneo la Bahi Sokoni.Picha na George John.

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto polisi wilaya ya Bahi amesema dawati hilo limekuwa likifanya kazi bila kujali upande kama anavyoeleza zaidi.

Sauti ya mkuu wa dawati la jinsia Bahi.

Baadhi ya wadau wengine walioshiriki mdahalo huo wamezitaja faida za kuacha kutelekeza familia huku wakibainisha kuwa baadhi ya wakati wilayani humo wanakabiliwa na umasikini unaotokana na tatizo hilo.

Sauti za wadau.