Dodoma FM

Vijana Bahi watakiwa kujiajiri

9 May 2023, 2:07 pm

Mafundi seremala Kiwanda kidogo Cha Msopo Camp wakiendelea na kazi kiwandani kwao.Picha na Bernad Magawa.

Mtaji wa kutosha kwaajili ya kuendesha kiwanda hicho unatajwa kuwa changamoto kwa vijana hao.

Na Bernad Magawa

Ili kupunguza tatizo la kukosekana kwa ajira za kutosheleza vijana wote wenye sifa za kuajiriwa hapa nchini, mafundi Seremala wilayani Bahi wamewaasa vijana kujiajiri wenyewe ili waweze kujikimu kiuchumi badala ya kusubiri ajira za serikali.

Wakizungumza na kituo hiki kilipotembelea ofisini kwao wamesema uamuzi wa kuanzisha kiwanda kidogo cha Samani za ndani umewanufaisha wao na jamii kwa ujumla kwani kimewawezesha kujikimu kikamilifu na familia zao.

Sauti ya Medhod Magubi .
Mafundi seremala Kiwanda kidogo Cha Msopo Camp wakiendelea na kazi kiwandani kwao.Picha na Bernad Magawa.

Aidha wameeleza mapokeo yao kwa jamii inayowazunguka huku wakitanabasha namna Halmashauri ya wilaya ya Bahi inavyoendelea kuwaunga mkono kwa kuwashirikisha kutengeneza samani za miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani humo.

Sauti ya Simon Damiani.

Mafundi hao wanasema kukosekana kwa mtaji wa kutosha imekuwa changamoto ya wao kukuza kiwanda chao ambacho ndipo walipowekeza maisha yao na kuiomba serikali pamoja na Taasisi mbalimbali za kifedha kuwaunga mkono.

Sauti ya Joseph Jumbe – Fundi Seremala.