Dodoma FM

Tamko la serikali kuelekea siku ya wanawake

6 March 2023, 4:52 pm

Dkt. Doroth Gwajima wakati akitoa tamko la serikali kuelekea siku ya kimataifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.Picha na Martha Mgaya

Elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi na kiutawala ili kuimarisha usawa wa kijinsia nchini.

Na Fred Cheti.

Serikali imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi na kiutawala ili kuimarisha usawa wa kijinsia nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalumu Dkt. Doroth Gwajima wakati akitoa tamko la serikali kuelekea siku ya kimataifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Machi mwaka huu.

Sauti ya Dkt. Doroth Gwajima.

Aidha Mh. Gwajima amesema kuwa serikali itahakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa wanawake na wasichana katika teknolojia ya mtandao ili kufikia usawa wa kijinsia katika maendeleo unaletwa kidigitali.

Sauti ya Dkt. Doroth Gwajima.

Kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbuka na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijami.