Dodoma FM

Bahi: Wakandarasi watakiwa kukamilisha, kukabidhi miradi ya maendeleo Juni 15

14 June 2023, 1:14 pm

Kamati ikikagua ujenzi wa shule mpya ya Nagulo Bahi.Picha na Bernad Magawa.

SSP Idd Abdala amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu, hivyo ni vema miradi yote ikakamilika kwa wakati.

Na Bernad Magawa.

Serikali wilayani Bahi mkoani Dodoma imewaagiza mafundi wote wanaojenga miradi ya maendeleo miundombinu ya elimu kwa fedha za BOOST kukamilisha na kukabidhi miradi hiyo mapema Juni 15, 2023 huku akiahidi kuchukua hatua kali kwa wote watakaoshindwa kukabidhi miradi hiyo.

Akitoa maagizo hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bahi wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo Juni 13, Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Bahi SSP Idd Abadalah amesema muda waliokubaliana na wakandarasi wanaojenga miradi hiyo tayari umepita hivyo wajitahidi kukamilisha.

Sauti ya Mkuu wa jeshi la Polisi wilaya ya Bahi SSP Idd Abadalah .
Kamati ya ulinzi na usalama ikikagua mradi wa madarasa ya Boost shule ya msingi Bahi Sokoni.Picha na Bernad Magawa.

SSP Idd Abdala amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu, hivyo ni vema miradi yote ikakamilika kwa wakati.

Kwa upande wao baadhi ya mafundi na viongozi wa vijiji wameahidi kuyatekeleza maagizo hayo kwa kufanya kazi usiku na mchana ili waweze kuendana na muda.

Sauti za mafundi na viongozi wa vijiji.