Wafanyabiashara Dodoma watakiwa kwenda maeneo waliyotengewa
7 July 2023, 5:27 pm
Mara kadhaa Dodoma Tv imeshuhudia baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia mgambo wa jiji kuwafukuza katika maeneo ambayo wamekatazwa kufanya biashara ambapo mara kadhaa halmashauri ya jiji imekuwa ikiwataka kuhamia katika maeneo waliyopangiwa.
Na Thadei Tesha.
Wafanyabiashara wanaofanya biashara katika eneo lilopo pembezoni mwa soko kuu la majengo jijini Dodoma wametakiwa kuacha kuendelea kufanya biashara katika maeneo hayo na badala yake kueleka katika maeneo mbalimbali waliyotengewa kwa ajili ya kufanyia shughuli hizo.
Mara kadhaa wafanyabiashra katika maeneo mbalimbali yanayozunguka barabara ya soko kuu la majengo ikiwa ni pamoja na eneo la bendera wamekuwa wakizuiliwa kufanya biashara katika maeneo hayo huku wakilalamikia mgambo wa jiji kuchukua bidhaa zao.
Hapa Bw Godson Rwegazama mwenyekiti wa soko kuu majengo anaeleza sababu ya kuchukua Hatua hiyo.
Hata hivyo amewataka kufanya biashara katika maeneo yaliyoelekezwa ikiwemo soko la Nkuhungu,kikuyu,na maeneo mengine yaliyotengwa ili kuepukana na changamoto za mara kwa mara za kufukuzwa kwa wafanyabiashara hao.