Dodoma FM

DC Kongwa: Ni haki ya wananchi kujua mapato na matumizi

22 May 2023, 4:41 pm

Mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kitongoji cha Morisheni Kongwa. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Wananchi wametakiwa kuhoji jambo lolote kwa viongozi wao ambalo hawalielewi ili waweze kupatiwa ufumbuzi.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amewataka wananchi, wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha wanahudhuria mikutano ya baraza la madiwani ili kujua mapato na matumizi ya halmashauri yao.

 Dkt. Nkullo ameeleza hayo katika mkutano wa wananchi wa kitongoji cha Morisheni alipotaka kujua changamoto zao ambapo katika mkutano huo ndugu Noel Milimo wa Kongwa alihoji juu ya ushiriki wa wananchi katika mikutano ya kusoma taarifa za mapato na matumizi.

Sauti ya  Dkt. Nkullo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kongwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Kongwa Mh. White Zuberi amesema serikali imewapatia bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa halmashauri mpya ambapo baada ya ujenzi huo kukamilika majengo ya halmashauri ya zamani yatatumika kama chuo cha afya.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kongwa.
Wananchi wa kitongoji cha Morisheni wakiwa katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mkuu wa wilaya Kongwa. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Mheshimiwa Zuberi amesema ni fahari Kwa wananchi wa kata ya Kongwa kuwa na hospital ya rufaa pamoja na kituo cha afya kinachotoa huduma nzuri katika maeneo ya karibu.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kongwa.

Akifunga mkutano huo mkuu wa wilaya Kongwa Mh. Remidius Mwema Emmanuel amewahakikishia wananchi ulinzi na usalama pia amehimiza viongozi ushirikishaji wa taarifa za maendeleo na wananchi kuendelea kuhoji juu ya jambo lolote ambalo hawalielewi.

Sauti ya mkuu wa wilaya Kongwa .