Dodoma FM

Serikali kuanza utelekelezaji wa mradi wa maji bwawa la Farkwa

21 March 2022, 1:54 pm

Na; Mariam Matundu.

Katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji mkoani Dodoma serikali imesema iko mbioni kuanza utekelezaji wa mradi wa maji wa bwawa la Farkwa .

Akizungumza na  taswira ya habari mkurugenzi wa bonde la wamiruvu kutoka wizara ya maji bwana Elibariki Mmassy amesema tayari wizara imepokea fedha kwa aajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Bwana Mmassy amesema serikali ya awamu ya sita imejidhatiti kuwekeza katika sekta ya maji ambapo wanatarajia kupokea mitambo 25 itakayosambazwa kila mkoa kwa ajili ya uchimbaji wa visima.

Aidha amesisitiza wananchi wanaotaka kuchimba visima kuomba vibali wizara ya maji ili wataalamu wadhibitishe eneo analotaka kuchimba kwa usalama wa watumiaji wa maji hayo.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za watu waliochimba visima bila kuomba kibali kutoka wizarani na kwamba kila atakaeisaidia wizara kupatikana kwa watu wanaochimba visima bila kufuata utaratibu watapata zawadi ya sh elfu hamsini.