Dodoma FM

Wakazi wa Gulwe wakosa mawasiliano ya simu

27 October 2022, 10:35 am

Na; Victor Chigwada.

Changamoto ya mawasiliano katika Kijiji Cha Gulwe imeendelea kuwaathiri wananchi kutokana na uhaba wa minara ya mitandao ya simu.

Wananchi hao wa Gurwe wamesema kuwa wamekuwa wakipata wakati mgumu wanapo hitaji kufanya mawasiliano kwa njia ya simu za mkononi

.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Wiliam Jonathan amekiri changamoto hiyo kuwaathili kwa kiasi kikubwa kwani wanalazimika kutafuta sehemu zinazoweza kuwasaidia kufanya mawasiliano

.

Naye Diwani wa Kata hiyo ya Gurwe Bw.Gabrieli Msaka ameiomba mamlaka husika kwa kushirikiana na wa miliki wa mitandao ya mawasiliano kufanya jitihada za kuongeza minara ya mawasiliano

.

Huduma ya mawasiliano hususani simu za mkononi imekuwa na watumishi wengi nchini na duniani kote na hivyo kupelekea taarifa nyingi kusambaa kwa njia ya simu za mkononi

Hivyo Ni vyema makampuni na wamiliki wa mitandao kufanya tafiti za namna ya kuboresha huduma ya mawasiliano kwa wateja wao