

4 April 2024, 5:39 pm
Katika kipindi cha miaka 3kuanzia 2021-2024 miche 113,306 imeweza kuzalishwa.
Na Fred Cheti.
Halmshauri ya jiji la Dodoma imefanikiwa kuongeza uzalishaji wa zao la zabibu ambalo ndio zao kuu la kimkakati katika jijini la Dodoma .
Hayo yameelezwa na bi Yustina Munishi mkuu wa divisheni ya kilimo katika halmashauri ya jiji la Dodoma wakati akifanya Mahojiano na kituo hiki kuhusu mafanikio yalipopatikana katika sekta ya kilimo ndani ya jiji la katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Rais Samia Madarakani.
Aidha katika hatua nyingine Bi Justina amesema kuwa halmshauri imeweza kuongeza huduma za ugani kwa kutoa vitendea kazi kwa maafisa kilimo ambapo jambo hilo limesaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula katika jiji la Dodoma .