Dodoma FM

Wanandoa watakiwa kuimarisha upendo kuepusha ndoa nyingi kuvunjika

23 May 2023, 4:56 pm

Picha ya mikono ya wanandoa ambao tayari wamekwishafunga pingu za maisha. Picha na Mwananchi.

Wazazi wametakiwa kuimarisha upendo na kuepuka kuvunja ndoa ambazo huacha watoto wakitaabika bila malezi huku wengine wakibaki kuwa watoto wa mitaani.

Na Bernad Magawa.

Ili kuhakikisha kuwa watoto katika familia wanalelewa na wazazi wote wawili, Wanandoa wameshauriwa kuimarisha upendo kati yao na kuhakikisha wanatatua kwa amani migogoro inayojitokeza ndani ya ndoa ili kupunguza wimbi la ndoa nyingi kuvunjia .

Baadhi ya wazee wilayani Bahi wakizungumza na kituo hiki wameshauri taasisi ya ndoa kuendelea kuheshimiwa, huku wanandoa wakiaswa kuvumiliana na inapobidi kuachana basi taratibu za kisheria zifuatwe ili kama kuna watoto waweze kupata stahiki zao kisheria.

Sauti za wazee.

Wazee hao wameishauri jamii kuzingatia maadili wanapooa au kuolewa kwani ni fedheha kwa mtu mwenye umri mkubwa sana kuoa au kuolewa na mtoto kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kiafrika.

Aidha wametoa rai kwa taasisi zote za dini pamoja na serikali kusimamia vema ustawi wa familia ili kunusuru mtikisiko mkubwa uliyopo katika familia nyingi kwa sasa.

Sauti za wazee.