Dodoma FM

Siku miamoja za uongozi wa rais Samia ,wachambuzi na wananchi wazungumzia maendeleo katika nyanja mbalimbali

29 June 2021, 12:07 pm

NA; SHANI NICOLOUS .

Kufuatia siku mia moja za Mh. Rais Samia Suluhu Hassan baadhi ya wananchi wamekuwa wakizungumzia kwa marefu na mapana maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza na Dodoma fm mchambuzi wamasuala ya kisiasa jijini Dodoma Bw. Jawadu Mohammed amesema kuwa ameonekana akifanya mambo mengi hususani upande wa kodi katika biashara, kufungua uhusiano na mataifa mengine na masuala mengi yenye tija kiuchumi nchini.

Amesema kuwa masuala ya kisiasa yameonekana kuboreshwa zaidi kwa kuteua nafasi za uongozi kwa watu mbalimbali bila kuangalia chama gani anatoka ili mradi anafaa katika kuleta maendeleo ya nchi hivyo ni mwanga mzuri wa umoja na mshikamano kupitia vyama vya siasa.

Bw. Abeli Majiko ni mkazi wa jiji la Dodoma yeye amesema kuwa ni tasfiri nzuri inayoonekana nchini tangu uongozi wa Rais Samia pamoja nakwamba watu walitengeneza imani finyu kwake kwakuwa ni Rais wa kwanza mwanamke kuongoza Nchini.

Raisi Samia amekuwa akikutana na makundi mbalimbali katika jamii nchini kuainisha vipaumbele vya serikali yake na pia kusikiliza maoni ya makundi hayo, ambapo mpaka sasa amekutana na kuzungumza na wazee,viongozi wa dini, wanawake,wafanyabiashara,vijana na watendaji wa sekta ya habari,huku akitimiza masuala kadhaa yaliyogusa nyoyo za Watanzania.