Dodoma FM

Ukosefu wa ajira chanzo cha matumizi ya dawa za kulevya

16 March 2022, 1:43 pm

Na; Elizabeth Japhet.

Ukosefu wa ajira unatajwa kuwa moja ya sababu inayosababisha baadhi ya vijana kujihusisha na utumiaji wa  dawa za  kulevya.

Bwana Swaleh ni miongoni mwa wahanaga wa dawa za kulevya na mfanyabiashara  wa soko kuu la majengo jijin Dodoma amesema vijana kutokujishughulisha na kazi kunasababisha kujiunga na makundi mabaya na kujihusisha katika  matumizi ya dawa za  kulevya.

Aidha mfanyabiashara huyo amesema kuwa baadhi ya wazazi wanawatenga watoto wao hivyo husababisha  vijana kujiunga na makundi  yanayojihusisha na  utumiaji wa dawa za kulevya  kutokana na upweke wanaoupata kwa wakati huo.

Kwa upande wake mshauri wa waathirika wa dawa za kulevya Bwana Christian Mlelwa kutoka jijini Dodoma  amesema ni muhimu wazazi kufatilia hatua kwa hatua  mienendo ya vijana wao ili kuwaepusha na matumizi ya dawa za  kulevya.

Matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana inachangia kuzorotesha  maendeleo ya kiuchumi ndani yaTaifa ambapo  Serikali inaendelea kupambana kuzuia uuzaji na  matumizi ya dawa za kulevya nchini.