Dodoma FM

Tume ya Taifa ya umwagiliaji imesema itaendelea kujenga miundonu pamoja na mabwawa ya kutunza maji

8 December 2021, 1:07 pm

Na;Mindi Joseph.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imesema itaendelea kukabiliana na maadiliko ya tabianchi kwa kutumia teknolojia zinazotumia maji kidogo na kujenga miundombinu pamoja na mabwawa ya kutunza maji.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Bw. Daudi Kaali amesema mabadiliko ya tabianchi yamekuwa na athari kubwa hivyo tume hiyo imejipanga kuhakikisha Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula na kuwahimiza wakulima kuzingatia kutunza mazingira katika vyanzo vya maji.

Bw. Kaali amesema kwa sasa mwamko wa wakulima kujishughulisha na shuguhli za kilimo cha umwagiliaji umekuwa mkubwa tofauti na ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.

Baadhi ya wakulima Jijini Dodoma wameipongeza tume ya Taifa ya umwagiliaji kwa kazi kubwa inayofanya katika kuhakikisha wakulima wananufaika huku wakiomba tume hiyo kuendelea kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepata mafanikio katika miaka 60 ya uhuru kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kwa zaidi ya hekta laki sita na tisini na nne kutoka hekta 1000 pekee kabla ya uhuru.