Dodoma FM

Baraza la Madaktari Tanganyika laridhia kufanyika kwa mtihani maalum kwa wanafunzi wa udaktari

23 October 2021, 3:23 pm

Na;Mindi Joseph .

Baraza La Madaktari Tanganyika limeridhia na kuruhusu kufanyika kwa Mtihani Maalumu Kwa Wanafunzi Wa Udaktari Wanaotarajia Kujiunga Na Utarajali Huku Nafasi Hiyo ikilenga tu wale Waliokutana Na Changamoto Wakati Wakifanya Usajili Lakini Hawakuwa Na Vigezo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma Mwenyekiti Wa Baraza La Madaktari Tanganyika Prof. David Ngassapa amebainisha kuwa Wanafunzi ambao walisoma Nje Ya Nchi Na Kushinda Kumaliza Kutokana na Changamoto Ya Uviko 19 Kuwasiliana Na vyuo hivyo ili Kukamilisha Masomo:

Aidha Baraza Hilo limesisistiza Kuwa Hakuna Mwanafunzi aliyefanya mitihani hiyo na akafeli kisha Kufaulishwa Kama Taarifa Zinavyosambazwa;

Tarehe 13 mwezi wa 10 2021 baraza la Madaktari Tanganyika lilitahini watarajali watarajiwa kutoka katika vyuo mbalimbali nchini vipatavyo 9 na wanafunzi kutoka nje ya nchi waliojiandikisha kufanya mtihani walikua 1242 na waliofanya mtihani walikuwa jumla 1,198 ambapo 1161 walikuwa wahitimu wa udaktari 36 wahitimu wa udaktari wa meno na mmoja muhitimu wa fiziotherapia.