Dodoma FM

Jamii yatakiwa kushirikiana na wataalam kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi

19 July 2023, 11:10 am

Mbunge wa Mbinga Vijijini Mhe. Benaya Kapinga akizungumza katika kikao hicho na wadau wa Ardhi. Picha na Wizara ya Ardhi.

Itakumbukwa kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji unaotekelezwa na mradi Uboreshaji wa Milki Salama za Ardhi,  ni wa miaka ishirini (20) ijayo kuanzia mwaka huu 2023 mpaka 2043 ukiwa na lengo kuu la kusimamia matumizi ya ardhi na kuimarisha ukuaji wa uchumi wa watu wanaoishi katika halmashauri za wilaya kwa kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ardhi na kuzingatia uhifadhi wa mazingira.

Na Seleman Kodima

Jamii imetakiwa kuendelea kushirikiana na wataala wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na halmashauri nchini  katika utekelezaji wa hatua zinazofuata za utekelezaji wa mradi wa mradi wa Uboreshaji wa milki salama za ardhi, ambazo ni kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji, upimaji wa vipande vya ardhi na kutoa hatimiliki za kimila.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mbinga, Pendo Ndumbaro ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziz Mangosongo wakati wa kikao cha wadau kujadili Rasimu ya mpango wa matumizi ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambapo amesema kupitia Mpango huu utumike kumaliza migogoro ya matumizi ya ardhi na migogoro ya mipaka ya vijiji, huku Mpango huu uwe  dira ya Matumizi sahihi ya kila kipande cha ardhi ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.

Aidha amesema kuwa Mpango huo Uanishe na kutoa njia sahihi za kusimamia utunzaji wa maeneo ya hifadhi za vilele vya milima, misitu na vyanzo vya maji na  ukiweka maeneo ya kimkakati ya uwekezaji kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.

Kwa Upande wake Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini –Kupitia Mradi huo Bw John Osena amesema mradi huo ni shirikishi baina ya wananchi kwa wananchi hivyo ni muhimu kutoa ushirikiano kwa wataalamu ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.

Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini –Kupitia Mradi huo .
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga, Pendo Ndumbaro ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziz Mangosongo wakati wa kikao cha wadau kujadili Rasimu ya mpango wa matumizi ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.Picha na Wizara ya Ardhi.

Nae Mbunge wa Mbinga Vijijini Mhe. Benaya Kapinga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuchukua maoni ya wabunge na kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ambapo sasa maeneo mengi yamefikiwa na mradi huo ikiwamo na Wilaya ya Mbinga

Sauti ya Mbunge wa Mbinga Vijijini Mhe. Benaya Kapinga .