Dodoma FM

Wananchi waiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya kujikinga na majanga

19 January 2022, 2:49 pm

Na; Thadei Tesha.

Baadhi ya wananchi jijini hapa wameiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na majanga mbalimbali ya asili.

Hayo yanajiri kufuatia hivi karibuni kutokea tetemeko la Ardhi katika baadhi ya maeneo ambapo lilileta taharuki kwa baadhi ya wananchi.

Wamesema bado elimu juu ya Namna ya kupambana na majanga hayo imekuwa ndogo kwa wananchi.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha majanga ya asili ya jiolojia Gabriel Mbogonyi  Amesema tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 5.5 katika kipimo cha Mita ambalo lilitokea Saa 7:27 usiku wa kuamkia jana ambapo pia amebainisha hatua mbalimbali za kuchukua pindi majanga hayo yanapojitokeza katika jamii.

Usiku wa kuamkia jana tetemeko la Ardhi limejitokeza jijini hapa ambapo wataalamu mbalimbali wanasema mgandamizo hupelekea tetemeko la Ardhi.