Dodoma FM

Ushindani katika ndoa chanzo wanaume kutowajibika

20 March 2023, 3:35 pm

Wanaume kutowajibika katika malezi na matunzo ya familia zao.Picha na wikipedia

Kukosekana kwa upendo na uaminifu limetajwa kuwa chanzo kikubwa Cha wanaume kutowajibika katika malezi na matunzo ya familia zao.

Bernadetha Mwakilabi.

Tukiwa katika mwezi wa wanawake kukosekana kwa upendo na uaminifu limetajwa kuwa chanzo kikubwa Cha wanaume kutowajibika katika malezi na matunzo ya familia zao.

Hayo yameelezwa na wadau wa masuala ya ndoa wilayani Kongwa walipokuwa wakijadili sababu hasa zinazopelekea baadhi ya wanaume kutowajibika katika familia, Anjela Beiya Helena Mbogo ni wadau wa ndoa ,hapa wanaeleza.

Sauti ya Anjela Beiya.

Sambamba na hayo utafutaji wa pesa kwaajili ya kutunza familia kwa wanawake imeonekana ni Ukosefu wa heshima kwa ndoa zao suala ambalo limepingwa vikali na wanawake.

Sauti ya Helena Mbogo.

Nao wanaume wameelezea sababu kubwa ya wao kuonekana hawawajibiki katika familia kuwa ni ushindani wa kiuchumi unayofanywa na wanawake.

Sauti ya mwanaume