Dodoma FM

Wanawake Bahi watakiwa kusimamia maadili ya watoto

18 July 2023, 12:52 pm

Mbunge wa jimbo la Bahi Kenneth Nollo akikabidhiwa tuzo na katibu wa UWT wilaya ya Bahi hilda mdaki. Picha na Bernad Magawa.

Mbunge wa Bahi amesema kipaumbele chake ni kuhakikisha afya ya mama na mtoto inakuwa salama.

Na Bernad Magawa.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Fatuma Taufiq amewaasa wanawake wilayani Bahi kusimamia maadili ya watoto ili kutokomeza viashiria vya maadili mabovu yanayopelekea uwepo wa ndoa za jinsia moja na unyanyasaji wa kijinsia.

Akizungumza kupitia baraza la wanawake wa CCM wilaya ya Bahi (UWT) Mheshimiwa Taufiq pia amewakumbusha kinamama kuwasaidia wasichana waliopata ujauzito wakiwa shule  warudi masomoni ili wapate fursa ya kutimiza ndoto zao.

Sauti ya Mheshimiwa Taufiq.

Naye Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bahi Imakulata Masigati akizungumza katika baraza hilo ameahidi kushirikiana na wanawake wilayani humo katika kazi za maendeleo.

Sauti yaMwenyekiti wa UWT wilaya ya Bahi.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bahi akizungumza wakati wa Baraza. Picha na Bernad Magawa.

Akieleza namna anavyopambana kuboresha miundombinu ya afya wilayani Bahi ili kuwahakikishia usalama wanawake wakati wa kujifungua, Mbunge wa jimbo la  Bahi Mheshimiwa Kenneth Nollo ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika baraza hilo amesema kipaumbele chake ni kuhakikisha afya ya mama na mtoto inakuwa salama.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la  Bahi Mheshimiwa Kenneth Nollo.