Dodoma FM

Wananchi walalamika kutolipwa fidia mradi wa bwawa Nagulo na Uhelela

4 September 2023, 1:56 pm

Picha ikionyesha mradi huo wa uchimbaji bwawa ukiendelea katika vijiji hivyo vya Uhelela na Nagulo. Picha na Thadei Tesha.

Kwa kujibu wa viongozi hao wanasema kuwa mradi huu ulianza tangu mwaka 2021 ambapo lengo ni kuwasaidia wananchi wa eneo hilo kufanya shughuli ndogondogo za kilimo ikiwemo mbogamboga.

Na Thadei Tesha.

Wananchi katika kijiji cha Uhelela na Nagulo kata ya bahi wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wamelalamikia serikali ya kijiji hicho kuweka mradi wa bwawa la maji katika maeneo yao bila ya kulipwa fidia.

Ni takribani kilometa 60 kutoka Dodoma mjini hadi katika kijiji cha uhalela kata ya Bahi wilayani Bahi jijini Dodoma.

Nafika ndani ya kijiji hiki na kushuhudia shughuli ya ujenzi wa bwawa ukifanyika hapa baadhi ya wakazi wa eneo hili wanaonekana kuwa na malalamiko kuhusiana na mradi huu.

Je wanazungumziaje mradi huu?

Sauti za wananchi.
Picha ni wakazi wa kijiji cha Uhelela wakiongea na Dodoma Tv.Picha na Thadei Tesha.

Dodoma tv imewatafuta viongozi wa eneo hili akiwemo mwenyekiti pamoja na diwani wa kata ya Bahi Bw Agustino Ndunu hapa wanatolea ufafanuzi suala hili huku wakieleza historia ya mradi huo.

Sauti za viongozi wa kata ya Bahi.

Lakini je ni yapi malengo hasa ya mradi huu hapa Diwani wa kata ya Bahi anaeleza zaidi.

Sauti ya Agostino Ndunu.