Dodoma FM

Ukosefu wa shule wasababisha ndoa za utotoni

7 March 2023, 6:46 pm

changamoto kubwa ya elimu kutokana na kukosekana kwa majengo ya shule.Picha na Habari mseto blog

Kukosekana kwa shule ya msingi kijiji cha Kaza roho Kata ya Manzase Wilaya ya Chamwino imesababisha wanafunzi kuacha masomo na kuamua kuolewa katika Umri mdogo.

Na Victor Chigwada,

Imeelezwa kuwa changamoto ya kukosekana kwa shule ya msingi kijiji cha Kaza roho Kata ya Manzase Wilaya ya Chamwino imesababisha wanafunzi kuacha masomo na kuamua kuolewa katika Umri mdogo

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakizungumza na taswira ya habari wamekiri kukabiliwa na changamoto kubwa ya elimu kutokana na kukosekana kwa majengo ya shule na kuwalazimu wanafunzi kujifunzia kwenye miti.

Sauti ya wananchi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kaza roho Bw.Hamisi Msumi amekiri katika kijiji hicho watoto wanalazimika kuishia darasa la nne kutokana na changamoto ya kukosa majengo ya shule licha ya jitihada za ujenzi kuendelea.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kaza roho Bw.Hamisi Msumi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Manzase Bw.John Mika akizungumza jithada za kata hiyo kutatua changamoto hiyo amesema kuwa kwasasa wanakabiliwa na changamoto ya mabati ili kukamilisha vyumba vya madarasa walivyo vijenga kwa nguvu za wananchi.

Diwani wa kata ya Manzase Bw.John Mika.