Dodoma FM

Serikali yaahidi kutatua changamoto ya maji Chunyu

19 October 2022, 8:57 am

Na;Mindi Josph .

Serikali imeahidi kuchimba visima vya maji ili kutatua changamoto ya maji inayowakabili wananchi  wa kijiji cha chunyu wilayani Mpwapwa.

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamesema hadi sasa wanatumia maji chumvi ambayo sio salama kwa afya zao.

Clip1..Wananchi

Kufuatia changamoto hiyo Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Malima amesema Tayari serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuchimba visima vya maji katika kijiji hicho ili kutatua changamoto hiyo.

Clp2…Mbunge

Hadi sasa visima zaidi ya 8 vimeshachimbwa katika vijiji zaidi ya 4  wilayani humo  ili kutatua adha ya maji  kwa Wananchi na kupunguza   umbali mrefu kufuata  huduma hiyo .