Dodoma FM

Bahi: Gharama kubwa zachangia wakulima kususia kilimo cha mpunga

1 June 2023, 4:56 pm

Moja ya shamba la mpunga lililopo wilayani Bahi jijini Dodoma . Picha na Bernad Magawa.

Wakulima hao wameendelea kuiomba serikali kuwatafutia masoko ya uhakika .

Na Bernad Magawa

Baadhi ya wakulima wa mpunga wilayani Bahi wameshindwa kushiriki kikamilifu katika kilimo msimu uliopita wa kilimo kutokana na gharama kubwa za kilimo hicho pamoja na pembejeo.

Mpunga ndilo zao pekee linalolimwa kwa wingi makao makuu ya wilaya ya Bahi na kata za jirani, lakini kilimo hiki kimekuwa na changamoto nyingi zikiwemo gharama kubwa za kulimia pamoja na kukosekana masoko yenye tija kwa wakulima ili kujikwamua kwani wamekuwa wakiuza mazao yao kwa wachuuzi wadogowadogo .

Ubovu wa miundombinu ya mashamba, ni changamoto nyingine inayomfanya mkulima wa mpunga wilayani Bahi kulima kwaajili ya chakula na siyo kibiashara hivyo kushindwa kabisa kukua kiuchumi.

Sauti za wakulima.
Moja ya shamba la mpunga lililopo wilayani Bahi jijini Dodoma . Picha na Bernad Magawa.

Abia Silungwe ni afisa ugani anayefanya kazi ndani ya wilaya ya Bahi anatoa wito kwa wakulima kufuata maelekezo ya maafisa ugani ili kulima kibiashara zaidi na hatimaye waweze kuongeza pato lao.

Sauti ya Afisa ugani.