Dodoma FM

Chamwino waishukuru serikali ujenzi wa vyuo vya VETA

14 April 2023, 1:31 pm

Miongoni mwa vyuo hivi ni hiki kinacho jengwa katika kata ya mlowa Bwawani wilayani Chamwino. Picha na Alfred Bulahya.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatarajia kukamilisha ujenzi wa vyuo 25 vya Wilaya kwa kutumia nguvu kazi ya ndani yaani force account.

Na Alfred Bulahya.

Wananchi wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, wameishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA vya Wilaya ambao utatoa fursa za Wilaya kupaa kimaendeleo.

Miongoni mwa vyuo hivyo ni kile kinachojengwa katika Kijiji cha Mlowa Bwawani kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma

Wakazi wa Kijiji cha Mlowa Bwawani wamesema ujenzi wa Chuo hicho, utapunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira wilayani humo.

Sauti za wananchi

Nini siri ya chuo hicho kujengwa katika kata ya Mlowa Bwawani? diwani wa kata hiyo anaeleza.

Sauti ya Diwani

Naye mwenyekiti wa kijiji hicho anafafanua namna walifanikisha kupata eneo kwa ajili ya ujenzi huo.

Sauti ya Mwenyekiti Mlowa bwawani