Dodoma FM

Wanufaika Tasaf walalamika malipo kuchelewa

21 April 2023, 3:02 pm

Mratibu wa TASAF Kongwa Bwana Elias Chilemu akizungumza na wananchi. Picha na Halmashauri ya wilaya ya Kongwa.

Mpaka sasa miradi hiyo ipo katika hatua nzuri za utekelezaji kwani hadi kufikia julai mwaka huu wataanza kutekeleza awamu ya pili ya miradi hiyo.

Na Bernadetha Mwakilabi

Wanufaika wa mfuko wa kusaidia kaya masikini TASAF wilayani Kongwa wamelalamikia Kuchelewa kwa malipo ya kazi za ajira za muda za miradi ya kuchonga barabara, kuchimba visima vya maji na mabwawa.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanufaika hao wamesema ni wiki ya sita sasa tangu wameanza kutekeleza miradi hiyo ambayo wanalipwa shilingi 3000 kwa siku lakini mpaka sasa bado hawajalipwa.

Akiongea kwa niaba ya wanufaika wengine Bwana Emmanuel Chunga wa kata ya Hogoro amesema.

Sauti ya mnufaika

Mratibu wa TASAF wilaya ya Kongwa Bwana Elias Chilemu amekili kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo ofisi yake  inashugulikia na ametolea ufafanuzi.

Sauti ya Mratibu wa TASAF wilaya ya Kongwa
Wananchi wa vijiji vya Kinangali na Msingisa wilayani Kongwa wakitekeleza mradi wa kuchonga barabara.Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Pamoja na malalamiko hayo pia Chilemu amesema mpaka sasa miradi hiyo ipo katika hatua nzuri za utekelezaji kwani hadi kufikia julai mwaka huu wataanza kutekeleza awamu ya pili ya miradi hiyo.

Chilemu amesema katika wilaya ya Kongwa kuna jumla ya miradi 92 ambayo ilianza mwezi machi na kutarajiwa kukamikika mwezi June japo kuna changamoto mbalimbali wanazozipitia kutokana na kuchelewa kuanza kwa miradi hiyo.

Sauti ya Mratibu wa TASAF wilaya ya Kongwa