Dodoma FM

Kondoa watakiwa kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati

5 May 2023, 3:45 pm

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma akikagua miradi Wilayani Kondoa. Picha na Mindi Joseph.

Na Mindi Joseph.

Katibu Tawala Mkoa wa dodoma Bw. Ally Senga ameangiza ujenzi wa Miradi ya maendeleo ya kimkakati inayotekelezwa katika Halmashauri ya Kondoa Mji kukamlika ifikapo June 15 mwaka huu.

Ameyabainisha hayo baada ya kutemebelea Miradi hiyo ikiwemo shule, ujenzi wa maabara na ukarabati wa Hospital ya wilaya ya kondoa mji.

Amesema miradi hiyo inapaswa kutekelezwe kwa kuzingatia Thamani ya Miradi hiyo.

Sauti ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Ameongeza kuwa Ifikakpo June mwaka huu 2023 miradi hiyo iwe imekamilika.

Sauti ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Miradi Hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu ili itakapokamilika ikidhi vigezo.