Dodoma FM

RAS Dodoma aridhishwa na utekelezaji wa Miradi Bahi.

14 April 2023, 1:59 pm

Ras akikagua hospitali ya Wilaya ya Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Gugu ameeleza kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri.

Na Bernad Magawa.

Katibu tawala wa mkoa wa Dodoma Ally Gugu ameeleza kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Bahi huku akielekeza miradi yote hususani ile ya ujenzi ambayo amebaini mapungufu kufanyiwa maboresho haraka.

Ally Gugu ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Bahi na kutembelea Miradi mitano ya maendeleo ikiwemo Hospitali ya wilaya ya Bahi, ujenzi wa zahanati Nagulo Bahi, shule ya viziwi kigwe pamoja na shule za Bahi English Medium na shule ya msingi Mpamantwa Barabarani.

Gugu ameeleza kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri huku akiagiza jengo la zahanati ya kijiji cha Nagulo Bahi kuanza kutoa huduma za afya kwa haraka.

Sauti ya Ally Gugu – Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma
Jengo la zahanati ya Nagulo Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya  Bahi Athmani Masasi akizungumza katika ziara ya katibu tawala huyo, ameahidi kutekeleza maagizo yote ndani ya muda walioutoa. Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Nagulo, kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Bahi Dkt.

Kasimu kolowa ameeleza namna wananchi walivyoshiriki katika ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itawaondolea adha ya kutembea zaidi ya kilomita tisa kufuata huduma kituo cha afya Bahi.

Sauti ya Dr. Kasimu Kolowa – Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Bahi