Dodoma FM

Shule za msingi mbili Chamwino zapatiwa msaada wa madawati

12 October 2023, 12:19 pm

Picha ni baadhi ya Viongozi wa Taasisi ya AFNET ,Shirika la Fondation for civil Society na  Viongozi wa Serikali. Picha na Noah Patrick.

Mradi huo wa Majaribio ambao umetekelezwa na kikundi cha Ujirani Mwema katika kijiji cha Wilunze ni matokeo ya kamati za ufatiliaji na uwajibikaji  ngazi ya serikali za Vijiji ambapo Mradi huo umesimamiwa na Shirika la AFNET kwa Ufadhili wa Taasisi ya Foundation for Civil Society.

Na Selemani Kodima.

Kikundi cha Ujirani Mwema kutoka wilunze Wilayani Chamwino kimetoa  madawati 140,Meza 14,Viti 14 katika shule za Msingi Juhudi na Wilunze ikiwa ni jitihada ya  kusaidia kukabiliana na changamoto ya Madawati katika shule hizo.

Akizugumza katika Halfa ya makabidhiano iliyofanyika shule ya Msingi Wilunze na kuhudhuriwa na Viongozi wa Taasisi ya AFNET ,Shirika la Fondation for civil Society na  Viongozi wa Serikali ,Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bi,Johanitha amesema hatua utoaji wa madawati katika shule hizi ni utekelezaji wa mradi ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Million 12,7199,00

Akitoa Ufafanuzi wa  fedha hizo ,Bi Johanitha amesema Shule ya Msingi Wilunze wamepewa  Madawati 90,Meza 8 na Viti 8 huku  Shule ya Msingi Juhudi  madawati 50 meza 6 na viti 6 .

Sauti ya Bi,Johanitha.

Kwa upande wake Afisa Mradi kutoka Shirika la Foundation for Civil Society Nicholas Lekule amesema Shirika hilo walifanikiwa kupata Mradi wa majaribio ambao jamii wanakuwa na jukumu la kusimamia mradi katika hatua zote za utekelezaji.

Amesema hatua waliofanya kikundi cha Ujirani Mwema inatoa Taswira ya namna jamii inaweza kufanya kazi na kusimamia mradi na kuibua changamoto na kuitatua.

Sauti ya bw.Nicholas Lekule.
Picha ni Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakifurahia msaada huo wa madawati. Picha na Noah Patrick.

Pamoja na hayo amekipongeza kikundi hicho kwa kazi walioifanya na mategemeo yao ni kuona muitikio wa wafadhili wa mradi huo katika hatua zijazo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la AFNET Bi Joy Njelango ameishukuru Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa Ushirikiano Mkubwa katika utekelezaji wa Mradi  huo ambao umefadhiliwa na Wilden Ganzen ambapo Shirika la Foundation for civil Society uliichagua Taasisi ya AFNET kuwa sehemu ya Utekelezaji.

Bi Njelango ametaja Vigezo vilivyowekwa ili kufanikisha uchaguzi wa Kijiji ambacho kimetukia katika Mradi huo wa majaribio kuwa ni pamoja na Uwepo wa Uongozi Bora,Ushirikiano na kuweza kupata matokeo,

Sauti ya Bi Joy Njelango.
Picha ni Viongozi wa Taasisi ya AFNET ,Shirika la Fondation for civil Society na  Viongozi wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Noah Patrick.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Tukio hilo  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino ambaye aliwakilishwa na  Mwl Zaina Kishengwe ambaye ni afisa Elimu idara ya Elimu ya Msingi amezishukuru Taasisi hizo ikiwemo  FCS na AFNET pamoja na kikundi Ujirani mwema Msaada wa Madawati 140.

Amesema Halmashauri ya Chamwino inaupungufu wa madawati kwa asilimia 47.9 ambapo sawa na madawati yanayopatikana kwa sasa kwenye shule zote ndani ya Halmashauri hiyo.

Sauti ya Mwl Zaina Kishengwe.

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Wilunze wameshukuru kwa Hatua iliyofanywa na Kikundi hicho ya kuona umuhimu wa utatuzi wa changamoto ya madawati.