Dodoma FM

Serikali yatoa maagizo kukabiliana na el nino

14 October 2023, 1:56 pm

Picha ni Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . Dotto Biteko akiongea katika kikao hicho. Picha na Mariam Kasawa.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko kukabidhi Mpango wa Taifa wa Dharura wa kuzuia na kukabiliana na madhara ya El nino kwa mawaziri na viongozi waliohudhuria mkutano huo.

Na Mindi Joseph.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imetakiwa kuunda mfumo wa ujumbe mfupi utakaowafahamisha wananchi juu ya mvua za El nino na madhara yake zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akiongea katika kikao cha mawaziri kuhusu utekelezaji wa mpango wa taifa wa dharura wa kuzuia na kukabiliana na madhara ya el nino Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema madhara ya mvua hizi yanamgusa kila mmoja kwani yatasababisha mafuriko na kuharibu miundombinu.

Sauti ya Dkt.Doto Biteko .
Picha ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Molel akikabidhiwa Mpango wa Taifa wa Dharura wa kuzuia na kukabiliana na madhara ya El nino. Picha na Mariam Kasawa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama amesema ofisi ya waziri Mkuu imeshaanda mpango wa taifa wa kukabiliana na El Nino.

Sauti ya Mh.Jenista Mhagama .

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a amebainisha Matukio ya hali mbaya ya hewa yanayoendelea kuongezeka.

Sauti ya Dkt.Ladislaus Chang’a.