Dodoma FM

Waumini wa dini ya kiislamu washauriwa kuendelea kutenda mema

10 April 2023, 12:22 pm

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu. Picha na Yussuph Hassan.

Ramadhani ni mwezi mtukufu ambao Waislamu hutumia mwezi wa Ibada wakiwa wamefunga, moja ya nguzo za Uislamu.

Na Yussuph Hassan.

Waumini wa dini ya kiislamu mkoa Dodoma wameshauri kuendelea kuutumia mwezi wa mtukufu wa ramadhani katika kutenda mema na zaidi.

Akizungumza na taswira ya habari Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu amesema mwezi wa ramadhani ni siku za kuhesabika ni vyema kuzikimbilia siku hizo katika kufanya mengi ya ziada ya wema.

Sauti ya Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu .

Aidha amesema kuwa katika kumi hili la Ramadhani ni muhimu kuongeza bidii za na kutobweka katika kufanya ibada.

Sauti ya Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu .