Dodoma FM

Dc kongwa akerwa na ubadhirifu wa fedha 6,394,000/=

18 April 2023, 3:39 pm

Mkuu wa wilaya ya kongwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Nyerere na Hogoro .Picha na Benadetha Mwakilabi.

Katika taarifa iliyosomwa inaonyesha kiasi cha shilingi milioni 6,394,000 hazijathibitika matumizi yake

NA Bernadetha Mwakilabi, Kongwa

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel ameagiza ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Kongwa kufanya uchunguzi juu ya ubadhilifu wa fedha uliofanywa na mwenyekiti wa kijiji cha Hogoro.

Agizo hilo limetolewa mapema baada ya taarifa ya mkaguzi wa ndani kuonesha  kuwa kuna upotevu wa fedha za wananchi katika kijiji cha Hogoro uliofanywa na mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Stephano Mgube

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.

Pia Mwema amefafanua kuwa baada ya kubaini ukweli wa tuhuma hizo mtuhumiwa atafikishwa katika vyombo vya Sheria  kwaajili ya kuwajibishwa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.

Akisoma ripoti ya mkaguzi wa mahesabu kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Kongwa bi Jackline Kigwa amesema kiasi cha shilingi milioni 6,394,000 hazijathibitika matumizi yake.

Sauti ya mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Kongwa
Mkuu wa wialaya ya Kongwa Mh. Remidius Mwema. Picha na Halmashauri ya wialaya ya Kongwa.

Sambamba na hayo Mheshimiwa mwema amesema katika uongozi wake hatofumbia macho masuala ya ubadhilifu wa fedha Rushwa na ufisadi.

Sauti ya Mkuu wa wialaya ya Kongwa.