Dodoma FM

Wamiliki wa mafuta waahidi kutoa ushirikiano wa kusambaza mafuta

25 July 2023, 4:30 pm

Wamiliki hao wamesema kuwa wanafanya kazi saa 24 hadi siku za mapumziko ili kuhakikisha magari yanaingia na kutoka katika maghala kwa lengo la kuchukua mafuta na kuyasafirisha katika maeneo mbalimbali. Picha na Wizara ya Nishati.

Wamiliki hao wameiomba serikali iimarishe upatikanaji wa dola ili zisaidie katika biashara hiyo.

Na Fred Cheti.

Wamiliki wa maghala ya mafuta nchini wameihakikishia Serikali kuhusu upatikanaji wa mafuta wakisema wana  petroli na dizeli za kutosha  na wapo tayari kutoa ushirikiano wa kuyasambaza kwenye maeneo mbalimbali yenye uhitaji.

Wamiliki hao wameyasema hayo mara baada ya serikali kupitia waziri wa Nishati Mhe. January Makamba kufanya ziara ya kukagua maghala ya kuhifadhia mafuta ya Petroli na Dizeli

Sauti za wamiliki.
Mhe. January Makamba amefanya ziara ya kukagua maghala ya kuhifadhia mafuta ya Petroli na Dizeli.Picha na Wizara ya Nishati.

Wamiliki hao wamesema kuwa wanafanya kazi saa 24 hadi siku za mapumziko ili kuhakikisha magari yanaingia na kutoka katika maghala kwa lengo la kuchukua mafuta na kuyasafirisha katika maeneo mbalimbali huku wakiiomba serikali iimarishe upatikanaji wa dola ili zisaidie katika biashara hiyo.

Sauti za wamiliki.

Kwa upande wake waziri wa Nishati Mhe January Makamba amewapongeza wamiliki wa maghala hayo kwa kuendelea kutoa huduma hiyo huku akihaidi serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwao.

Sauti ya waziri wa Nishati.