Dodoma FM

Daraja jipya suluhisho kwa wakazi Nzali, Chilonwa

12 May 2026, 16:59

Daraja hilo ambalo litaimarisha mawasiliano kati ya Kijiji cha Chilonwa na Nzali Wilayani Chamwino.Picha na wizara ya ujenzi.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Dodoma mhandisi Zuhura Amani amesema kukamilika kwa daraja hilo kutamaliza changamoto ya mawasiliano ya muda mrefu katika barabara ya Chamwino- Dabalo Itiso -Chinene Km 70 ambayo inaunganisha barabara ya Morogoro na Arusha.

Na Victor Chigwada.

Kukamilika kwa daraja linalounganisha kijiji cha Nzali na Chilonwa imekuwa afueni Kwa wakazi wa vijiji hivyo na kuondoa adha ya muda mrefu ambayo walikuwa wakikutana nayo msimu wa mvua .

Wananchi hao wa kijiji cha Chilonwa wamesema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekuwa na tija Kwa wananchi kwani hapo awali shughuli mbalimbali za kijamii zilikuwa zikikwama ifikapo msimu wa mvua

Wananchi hao wameongeza kuwa hapo awali wakati hakuna daraja watu walikuwa wanakufa maji mara kwa mara hivi sasa daraja hilo litasaidia kuondokana na madhara mbalimbali.

Sauti za wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji Bw.Esau Lekadi ameishukuru Serikali Kwa kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ambapo hapo mwanzo ilikuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo.

Sauti ya Bw.Esau Lekadi.