Wananchi Chiponza walalamika kuchangia vyanzo vya maji na mifugo
21 July 2026, 16:42

Kwa mujibu wa sera ya maji kutoka wizara ya maji inasema maji ni muhimu kwa viumbe vyote duniani, bila maji hakuna uhai aidha maji ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ,kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote kina tegemea kuwepo kwa maji ya kutosha na yenye ubora unaotakiwa.
Na Anwary Shaban.
Wananchi wakitongoji cha Chiponzi, kata ya Makang’wa wilayani Chamwino wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama hali inayo walazimu kuchangia vyanzo vya maji na mifugo.
Wakizungumza na Taswira ya Habari wakazi wa kijiji hicho, wamesema uhaba wa maji umekuwa kero ya muda mrefu, na kwasasa wanategemea maji kutoka kwenye visima vichache vinavyo tumiwa pia na mifugo ya kijiji hicho .
Wananchi hao wameeleza kuwa hali hiyo si tu inahatarisha afya zao, bali pia inawaongezea mzigo wa kutafuta maji kwa umbali mrefu kila siku ili waweze kupata maji safi hivyo wanaiomba serikali kutatua kero hii ya maji katika eneo hilo.
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Makang’wa, Bi. Dina Menda, amesema kuwa uongozi wa kata umepokea malalamiko hayo ya wananchi juu ya uhaba wa maji na tayari wameiwasilisha kwa Mamlakaya Maji naUsafi wa MazingiraVijijini, Ruwasa.